.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Agosti 2016

DKT. SHEIN AFANYA UTEUZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, ACP Sida Mohammed Himid ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ anayeshughulikia Idara maalum za SMZ.

Ndugu Hassan Khatib Hassan ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto anayeshughulikia masuala ya Wazee, vijana, wanawake na Watoto.

Dkt. Ali Salim Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja katika Wizara ya Afya.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 30 Agosti, 2016 huku kwa Bw. Mohammed Kheir Mtumwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia tarehe 28 Agosti, 2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni