Kocha
Pep Guardiola atarejea Barcelona akiwa na Manchester City baada ya
klabu yake hiyo mpya kupangiwa kukutana na Barcelona katika droo ya
Ligi ya Mabigwa Ulaya.
Guardiola
ambaye alishinda mara mbili kombe la michuano hiyo akiwa na
Barcelona, aliiongoza City kufuzu kuwania kutinga katika michuano
hiyo kwa kuifunga Steaua Bucharest.
Timu
hizo zipo katika kundi la C, wakiwa pamoja na Borussia
Monchengladbach na Scottish champions Celtic.
MAKUNDI
YOTE YA UEFA YAMEPANGWA KAMA IFUATAVYO:-
KUNDI
A: Paris Saint-Germain, Arsenal, Basle na Ludogorets, KUNDI B:
Benfica, Napoli, Dynamo Kyiv na Besiktas, KUNDI C: Barcelona,
Manchester City, Borussia Monchengladbach na Celtic, KUNDI D: Bayern
Munich, Atletico Madrid, PSV Eindhoven na Rostov.
Aidha, katika hafla hiyo UEFA imemtangaza mshambuliaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuwa mwanasoka bora wa UEFA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni