Uhamisho wa golikipa Claudio Bravo
kwenda Manchester City umekamilika na kufungua milango kwa Joe Hart
kuondoka dimba Etihad katika msimu wa majira ya joto.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile,
amethibitishwa kujiunga na City saa chache baada ya Barcelona
kuthibitisha kumpata mrithi wake Jasper Cillessen kutoka Ajax.
Manchester City imetoa kitita cha
paundi milioni 17 kumnasa Bravo kufuatia uamuzi wa Pep Guardiola
kumtosa Joe Hart.
Claudio Bravo akitua Manchester hii leo tayari kwa ajili ya kufanyiwa vipimo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni