Jeshi la Polisi Zanzibar limedhamiria kupambana na uharamia wa kazi za hakimiliki kwa kudhibiti maeneo ya uingizaji hakimiliki haramu katika maeneo ya bandarini na uwanja wa ndege .
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omari amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuhusu usimamizi na wajibu wa Jeshi la Polisi katika usimamizi wa hakimiliki .
Amewataka wananchi kuelewa kwamba kutoa kopi ,kuuza vinasa sauti na picha za kieletroniki vikiwemo CD,DVD na vyenginevyo bila ya leseni ya hakimiliki ni miongoni mwa makosa ya jinai.
Aidha alisema kutumia hakimiliki biila ya ridhaa ya mwenye haki kama vile kurudufu kusambasa na kuonyesha kazi kwa umma ama kuibadilisha kazi na kuwa kwa mtindo mwengine ni kosa kwa mujibu ya sheria ya hakimiliki No. 14 ya mwaka 2003.
Amesema hakimiliki ni mali ya anaemiliki ,ni kazi yake inaestahili ulinzi kwani kuitumia bila ya ridhaa ya mwenye haki ni kosa kisheria
Katika kusimamia sheria ya hakimiliki Jeshi la Polisi limetoa taaluma kwa askari wake wakiwemo makamanda wa mikoa yote ya Zanzibar katika mwaka 2008 -2009 ofisi ilianzisha kikundi kazi cha hakimiliki .
Alieleza kuwa jumla ya polisi 100 wa Unguja na Pemba walipatiwa mafunzo ya utambuzi wa makosa ya hakimiliki kupitia mtalamu wa utambuzi wa jinai za hakimiliki SP Omar Muwowo kutoka jeshi la polisi Zambia na Interpol.
Kamishna huyo alieleza kuwa Jeshi la Polisi lilifanikiwa kupambana na uharamia wa hakimiliki kwa kushirikiana na Afisi ya hakimiliki kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya Unguja na kukamata nakala haramu za vinasa sauti na picha vya kielektroniki vikiwemo CD , DVD‘S na MP3 zenye uzito wa tani mbili .
Aidha alisema nakala haramu hizo ziliangamizwa kwa kushirikiana na Idaraya Mazingira Zanzibar
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni