.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 25 Agosti 2016

MADIWANI KUTOKA UGANDA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM

mea1
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano baina ya Wataalamu kutoka Jijini la Dar es Salaam na Madiwani kutoka baadhi ya Halmashauri za Uganda Magharibi na Kaskazini wakati wa ziara yao ya kujifunza masuala mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Majiji Tanzania (TACINE) Bw. Philotheusy Mbogoro, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka ya Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson.
mea2
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano baina ya Wataalamu kutoka Jijini hilo na baadhi ya Madiwani kutkoka Halmashauri za Miji nchini Uganda wakati wa ziara yao ya kujifunza masuala mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka ya Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles
mea3
Afisa Uhusiano na Itifaki wa Jiji la Dar es Salaam Gaston Mwakwembe akielezea jambo wakati wa mkutano uliowakutanisha baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Jiji na baadhi ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Madiwani hao wapo katika ziara ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
mea4
Mhandisi wa Barabara wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Swalehe Nyenye akiwasilisha maada kuhusu mkakati wa kuboresha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam leo wakati wa ziara ya baadhi ya Madiwani kutoka Uganda walipo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
mea5
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Godhelp Ringo akifafanua maada kuhusu muundo wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya baadhi ya Madiwani kutoka Uganda waliopo nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
mea6
Baadhi ya Madiwani kutoka nchini Uganda wakifuatilia mada kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Barabara na Mitaa, Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
mea7
Baadhi ya Madiwani kutoka nchini Uganda wakifuatilia mada kutoka kwa wataalamu wa Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo Barabara na Mitaa, Menejimenti ya Usafiri, Uchafu, Maji, Rasilimali watu, Fedha,Kilimo cha mjini,na namna ya kuongoza mabaraza ya Madiwani.
mea8
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa.
mea9
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akipokea zawadi kutoka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa.
mea10
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita Charles akimkabidhi zawadi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Koboko, na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mamlaka za Miji nchini Uganda (UAAU) Mhe. Sanya Wilson(kushoto) wakati wa ziara ya Madiwani kutoka nchini Uganda leo Jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Kaimu ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam, Phillip Mwakyusa.  Picha na Frank Shija, MAELEZO.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni