Timu hiyo imekuja Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu wa ufukweni ambako itacheza na wenyeji Tanzania Ijumaa wiki hii kwenye uwanja maalumu ulioandaliwa kwa ajili ya mchezo huo.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na Muhammad Ssenteza.
Mtunza muda katika mchezo huo atakuwa Adil Ouchker wa Morocco huku Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi. Timu hizo zinatarajiwa kucheza mechi mbili za kuwania kufuzu kwani mara baada ya mchezo wa Dar es Salaam, zitarudiana tena Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Kwa upande wa Tanzania, Kocha Mkuu wa timu hiyo, John Mwansasu, anaendelea na mazoezi na wachezaji wake 16 aliowatangaza wiki iliyopita. Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji sita kutoka Zanzibar na 10 Tanzania Bara.
Wanaounda kikosi hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahmad, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa) Khamis Said na Yacob Mohamed wote kutoka Zanzibar.
Wengine ni Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma na Kevin Baraka.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni