Kocha Jose Mourinho ameridhia, Paul
Pogba, kuichezea kwa mara ya kwanza Manchester United baada ya
kujiunga tena na klabu hiyo ambapo kesho atakuwa kwenye kikosi
kitakachovaana na Southampton.
Mfaransa Pogba, 23, aliyehamia Old
Trafford kwa kitita cha paundi milioni 100 amefanya mazoezi na
Manchester United kwa muda wa chini ya wiki mbili, akitokea
mapumzikoni Marekani baada ya kumalizika michuano ya Euro 2016 nchini
Ufaransa.
Paul Pogba akifurahi jambo wakati wa mazoezi akiwa na Manchester United


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni