Mwanariadha Mjamaica Usain Bolt
ametwaa medali yake ya nane ya dhahabu katika michuano ya Olimpiki na
kuendelea kuonyesha ubabe wake katika Olimpiki Rio baada ya kushinda
mbio za mita 200.
Hata hivyo ushindi huo wa Usain Bolt
aliyetumia muda wa sekunde 19.78, haukumfurahisha kutokana na
kushindwa kuvunja rekodi ya muda wa kumaliza.
Bolt amebakiza mbio moja za mita 100
kwa watu wanne kupokezana kijiti, na kuweka rekodi kuwa mwanariadha
wa kwanza kushinda mbio za aina tatu mara tatu katika michuano ya
Olimpiki.
Mwanariadha Usain Bolt akielekea kumaliza mbio za mita 200
Mwanariadha Usain Bolt akipiga Selfie na mashabiki waliojitokeza kushuhudia mbio hizo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni