Watoto hao Saanchi Goyal, 3, na
Harry, 4, walikuwa wametoa vichwa vyao juu ya gari lenye uwazi juu ya
paa lake wakiangali maeneo tofauti ya Delhi na ndipo kamba ya kishada
ilipoyakata makoo yao.
Naye Zafar Khan, 22, alikufa kwa
ajali kama hiyo wakati akiendesha pikipiki yake na kujikuta koo lake
likikatwa na kamba kishada.
Kamba ziliyochanganywa na chupa
hutumika katika kukatiana vishada, lakini zimekuwa zikisababisha
majeruhi na vifo.
Raia wengi wa India hurusha vishada
katika kusherehekea sherehe mbalimbali muhimu kama vile sherehe za
uhuru ambayo huadhimishwa Agosti 15.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni