Hali ya kuogopesha inayoanisha janga
katika vita vya nchini Syria imejionyesha katika picha moja
iliyopigwa ikimuonyesha mtoto aliyejeruhiwa.
Picha hiyo inamuonyesha mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka 5, aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha gari
la wagonjwa baada ya mashambulizi nyumbani kwao Aleppo, huku hatma ya
wazazi wake walipo ikiwa haijulikani.
Akiwa amejaa mavumbi mwili mzima
baada ya kuokolewa kwenye vifusi vya nyumba yao iliyoshambuliwa
katika eneo moja la Omran Daqneesh, uso wa mtoto huyo uliokuwa
ukitiririka damu huku akiwa ameduwaa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni