Nchi
ya Kenya imeingia gizani kufuatia kukosekana kwa umeme karibu nchi
nzima kulikotokea leo asubuhi.
Taarifa
iliyotolewa na Shirika la Umeme la Kenya Power, tukio hilo limetokea
leo majira ya saa kumi na moja alfajiri, kufuatia kutokea kwa
hitilafu.
Hitilafu
hiyo imetokea katika njia kuu ya umeme ya 220KV huko Olkaria Jijini
Nairobi na kusababisha kukosekana umeme katika maeneo mengi ya Kenya.
Shirika
la Kenya Power limesema bado halijabaini chanzo cha hitilafu hiyo, na
haliwezi kusema kwa sasa ni wakati gani umeme utarejea tena.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni