Moto
uliotokea kwenye sherehe ya kuzaliwa iliyokuwa ikifanywa kwenye baa
kaskazini mwa Ufaransa katika mji wa Rouen umeuwa watu wapatao 13 na
kujeruhi wengine sita.
Mishumaa
kwenye keki ndiyo iliyosababisha moto katika baa hiyo ya Cuba Libre,
ulioanza majira ya usiku wa manane kuamkia leo.
Paa
la baa lililojengwa kwa kutumia plastiki ngumu lilishika moto wakati
sherehe hiyo ikiendelea kwa mujibu wa shirika la AFP.
Waziri
wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema zaidi ya
askari wa zimamoto 50 waliitwa kuzima moto huo.
Vikosi vya zimamoto vikiwa katika eneo la tukio baada ya kufanikisha kuuzima moto
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni