.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 6 Agosti 2016

SHAMRASHAMRA KIBAO ZAPAMBA UFUNGUZI WA MICHUANO YA OLIMPIKI 2016

Michuano ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2016 imefunguliwa rasmi kwa shamrashamra za aina yake Jijini Rio katika dimba la Maracana nchini Brazil.

Tukio hilo lililorushwa mubashara kupitia runinga kwa watu bilioni 3 duniani, liliambatana na kuonyesha historia, utamaduni na uzuri wa Brazil.

Katika ufunguzi huo mwanariadha wa zamani wa Vanderlei de Lima aliwasha Mwenge wa Olimpiki, na mwanariadha wa zamani Kenya Kipchoge Keino alinyanyua juu kombe la Olimpiki mwishoni wa sherehe hizo za ufunguzi.
Dimba la Maracana lilivyokuwa linaonekana wakati wa shamrashamra za ufunguzi wa michuano ya olimpiki
                  Kikundi cha dansi cha Samba kikitoa burudani wakati wa ufunguzi
   Burudani ya samba ikiendelea kutolewa wakati wa ufunguzi wa michuano ya Olimpiki
Rais wa mpito wa Brazil Michel Temer akihutubia wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo
   Mwanariadha wa zamani wa Brazil Vanderlei de Lima akiwasha Mwenge wa Olimpiki

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni