.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 29 Agosti 2016

KIPAO AMBADILI MUNISHI TAIFA STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa, amefanya mabadiliko kwenye kikosi kinachotarajiwa kusafiri Jumatano Agosti 31, 2016 kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles.

Mabadiliko yaliyofanyika ni kwa kumchukua Kipa kinda wa JKT Ruvu, Said Kipao kuchukua nafasi ya Deogratius Munishi ambaye amefiwa na baba yake mzazi katika kifo kilichotokea jijini Dar es Salaam jana Agosti 28, 2016.

Licha ya mchezo huo wa Septemba 3, 2016 kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho kwa sasa na kuanza kuingia kambini Hoteli ya Urban Rose jijini Dar es Salaam ni:

Makipa-

Said Kipao – JKT Ruvu 

Aishi Manula – Azam FC

Mabeki

Kelvin Yondani - Young Africans 

Vicent Andrew - Young Africans 
Mwinyi Haji - Young Africans 
Mohamed Hussein – Simba SC 
Shomari Kapombe - Azam FC 
David Mwantika - Azam FC

Viungo

Himid Mao - Azam FC 

Shiza Kichuya – Simba SC 
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC 
Muzamiru Yassin – Simba SC 
Juma Mahadhi - Young Africans 
Farid Mussa Tenerif ya Hispania

Washambuliaji

Simon Msuva - Young Africans 

Jamal Mnyate – Simba SC 
Ibrahim Ajib – Simba SC 
John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni