Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumitomo Corporation ya Japan, Bw. Kunihuru Nakamura katika Mkutano wa TICAD 6 uliofanyika Nairobi Kenya, Agosti 28, 2016. (Pivha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais na Ofisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sumimoto Corporation ya Japan katika mkutano wa TICAD 6 uliofanyika jijini Nairobi Agosti 28,2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Sumimoto ya Japan, Bw. Kanihuru Nakamura (kushoto kwake) baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa James Mdoe na Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt.Adelhelm Meru. Wanne kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mathias Chikawe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Wakimbizi, Fillipo Grand kabla ya mazungumzo yao jijini Nairobi, Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa kitabu chenye picha ramani na taarifa za jiji la Yokohama nchini Japan na Meya wa jiji hilo, Bi. Fumiko Hayashi baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa jiji la Yokohama nchini Japan , Bi. Fumiko Hayashi baada ya mazungumzo yao jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza , Bw. Lameck Borega (kushoto) ambaye ni Meneja wa Uwekezaji kutoka EPZA, Mabibo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama pipili iliyosindikwa na kupewa jina la AKABANGA wakati alipotembelea banda la Rwanda katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonyesho kutoka Senegal wakati alipotembelea bada lao kwenye maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nguo za batik wakati alipotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho yaliyokwenda sambamba na mkutano wa TICAD 6 jijini Nairobi Agosti 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni