Lionel Messi na Luis Suarez
wamerudisha makali yao ya kucheka na nyavu wakati wa kuelekea kuanza
msimu mpya baada ya kuisaidia Barcelona kuichakaza Sampdoria katika
kombe la Gamper.
Wenyeji timu ya Barcelona walianza
vizuri wakati Luis Suarez alipounganisha mpira uliopigwa kwa kwa
ufundi kwa kutumia staili ya tik taka na Lionel Messi na kuiandikia
Barcelona goli la kwanza.
Messi aliongeza la pili kwa
Barcelona dakika tano baadaye kabla ya Sampdoria nao kufunga goli
moja kupitia kwa Ante Budimir katika kipindi cha pili lakini Messi
tena aliongeza goli la tatu kwa mpira wa mkwaju wa adhabu.
Lionel Messi akikatiza kati kati ya wachezaji wa timu ya Sampdoria
Luis Suarez akichomoka na mpira katika mchezo huo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni