Wenyeji Brazil hatimaye wamezinduka
na kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Soka ya Olimpiki
kwa ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Denmark jana baada ya mabingwa
watetezi Mexico na mabingwa mara mbili Argentina kutolewa.
Baada ya kutoa sare katika michezo
yake miwili ya kwanza Brazil, ilikuwa inahitaji ushindi ili kutuliza
hasira za mashabiki wa taifa hilo linalopenda soka mno,
walijihakikishia kutinga hatua hiyo kupitia kwa magoli ya Gabriel
Barbosa na Gabriel Jesus.
Luan na Barbosa waliongeza magoli
mengine mawili katika kipindi cha pili na kuifanya Brazil iongoze
kundi A, huku ikijianda kushuka dimbani jumamosi kwa mchezo wao dhidi
ya Colombia.
Gabriel
Barbosa akiangalia mpira alioupiga ukitinga wavuni
Gabriel Barbosa akiifungia Brazil goli la nne



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni