Kikosi imara cha Liverpool kimefanya
mauaji kwa Burton Albion na kutinga hatua ya tatu ya Kombe la EFL
mzunguko wa tatu, baada ya kuichakaza timu hiyo kwa kipigo cha magoli
5-0.
Wekundu hao walianza kuongoza katika
dakika ya 15 kupitia kwa Divock Origi kabla ya baadaye Roberto
Firmino kuongeza la pili 2-0 kwa kichwa akiunganisha krosi ya
Nathaniel Clyne.
Tom Naylor alijikuta akijifunga
mwenyewe na kuipatia Liverpool goli la tatu baada ya mapumziko na
kisha baadaye Daniel Sturridge kufunga mengine mawili.
Divock Origi akifunga goli baada ya kuunganisha pande kutoka kwa Sadio Mane
Roberto
Firmino akifunga goli la pili la Liverpool kwa mpira wa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni