.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 3 Agosti 2016

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NYAMA NA STENDI YA MSAMVU MOROGORO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiteremka kuelekea eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama Ngulu Hills Ranch kilichopo Morogoro wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakikagua eneo la kuchinjia ng'ombe katika kiwanda cha nyama cha Nguru Hills Ranch cha Morogoro Agosti 3, 2016. Kushoto ni Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda hicho, Danstan Mrutu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakizingumza na Mkurugenzi na mshauri wa kiwanda cha nyama cha Ngulu Hills Ranch cha Morogoro , Dunstan Mrutu (kulia kwa Waziri mkuu) ) wakati walipokitembelea kiwanda hicho Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Watoto na wananchi wa kijiji cha Majichumvi wilayani Mvomero wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa aliposimama kijijini kwao kuwasikiliza Agosti 3, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pesheni wa LAPF, Eliud Sanga wakati alipokagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Stendi mpya ya mabasi la Msamvu mjini Morogoro Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mjini Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa stendi mpya ya Msamvu Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt.Stephene Kebwe na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Eliud Sanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Awamu ya kwanza ya jengo la stendi mpya ya mabasi ya Msamvu mjini Morogoro iliyokamilika kwa asilimia 90. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliitembelea stendi hiyo na kuzungumza na wadau Agosti 3, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Halima Mwishehe alipouliza swali wakati Waziri Mkuu alipozungumza na Wananchi kwenye stendi mpya ya Msamvu Morogoro baada ya kukagua ujenzi wake Agosti 3, 2016. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni