Polisi
walioshehena silaha nzito maalum kwa ajili ya kufanya doria
wamesambazwa rasmi kwenye mitaa ya Jiji la London nchini Uingereza
hii leo baada ya wimbi la matukio ya mashambulizi ya ugaidi Ulaya.
Kamishina
wa polisi Sir Bernard Hogan-Howe amebainisha mpango ambao licha ya
kuweka askari wenye sare pia kutakuwa na askari kanzu wanaofanya
doria wakiwa na bastola na bunduki ya SIG Carbine rifles.
Mbali
na bunduki polisi hao wapya wa doria watakuwa na pikipiki aina ya BMW
F800GS ili kuwaruhusu kulifikia kwa urahisi eneo lolote na katika
Jiji Kuu kutakuwa na bodi za mwendo kasi zitakazokuwa zikifanya
doria.
Polisi maalum wa kupambana na ugaidi wakiwa na vifaa vyao kama vinavyoonekana katika maelezo kulingana na namba
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni