Timu
ya Manchester City imethibitisha kumnasa mshambuliaji wa Palmeiras,
Gabriel Jesus kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 27.
Ikiwa
ni baada ya saa 24 tangu kukamilisha uhamisho wa Leroy Sane kwa
paundi milioni 37 kutoka Schalke, City wamewapiku Barcelona na
kumnasa winga huyo Mbrazil Jesus, 19.
Kama
ilivyo kuwa kwa Sane, Jesus ambaye analiwakilisha taifa lake katika
michuano ya Olimpiki huko Rio amekubali mkataba wa miaka mitano, ila
atabakia Palmeiras hadi Krismasi, wakati msimu wa soka wa Brazil
utakapomalizika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni