Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam linaendelea kuwasaka kwa kasi majambazi waliofanya mauaji ya askari polisi wanne ( 4 ) usiku wa kuamkia leo katika eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema askari hao waliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi ambayo idadi yao bado haijajulikana wakati walipokuwa wakibadilisha lindo.
Kamanda Sirro amesema kwamba, askari hao wakiwa ndani ya gari la polisi aina ya Ashok, wakati wanateremka ili kubadilishaba lindo katika benki ya CRDB Mbande, ndipo majambazi hayo yaliyokuwa yamejificha sehemu yakaanza kuwashambulia kwa sirasi na kuwaua askari polisi wanne huku askari polisi mmoja aliyekuwa lindo katika benki hiyo akifanikiwa kukimbia eneo hilo na kusalimisha maisha yake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni