.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 30 Agosti 2016

MCHIMBA KISIMA AUWAWA NA MOTO WA MKAA ARUSHA

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo
Na Woinde Shizza, Arusha

Mchimbaji wa kisima aliyefahamika kwa majina ya Waziri Omary (25) mkazi wa  Ngaramtoni amefariki dunia kisimani wakati akichimba kisimani.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo  amekiri kutokea kwa tukio hilo marehemu alikutwa amefariki kisimani  baada ya kuwasha moto wa mkaa ili kulainisha mwamba ili aweze kupata maji kwenye kisima chenye urefu wa futi 60, alikutwa saa 5 juzi akiwa ameshapoteza maisha.

"Kilichotokea ni kwamba huenda wakati amewasha jiko, Carbonmonoxide ilizidi huku hewa ya Oxygen ilikuwa ndogo kiafya lazima angedhurika. Mwili wa marehemu haujakutwa na jeraha lolote, tunaendelea na uchunguzi kubaini zaidi , "alisema Kamanda. Pia amewatahadharisha watu kuhakikisha watu nawapotumia majiko ya mkaa ndani kuhakikisha kuna hewa ya kutosha.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni