Na Woinde Shizza,Arusha
Wakazi wa Jiji la.Arusha na vuiunga vyake pamoja na kutoka mikoa jirani wamefurika katika Tamasha linaloitwa LETS PRAISE SUMMIT, lililoandaliwa na Mchungaji Adamu Haji katika Kituo cha kimataifa cha Mikutano (AICC) katika ukumbi wa Simba.
Maelfu ya watu hao walianza kumiminika katika Kituo hicho cha Mikutano kuanzia saa tatu asubuhi ambapo hata kabla tamasha hilo halijaanza tayari Ukumbi wa Simba uliopo AICC ulikuwa umejaa na hivyo kusababisha maelfu ya watu waliofika kuzuiliwa nje kwa kuwa kulikuwa hakuna namna ya wao kuingia ukumbini kutokana na kufurika kwa watu.
Akielezea hali hiyo ya maelfu ya wahudhuriaji wa tamasha kushindwa kuingia ukumbini, Muandaaji wa tamasha hilo mchungaji Adamu Haji amesema kuwa hakutegemea kuwa watu wangelikuwa na muitikio mkubwa namna hiyo hivyo amesema kuwa atamuomba muimbaji huyo asiondoke mapema ili lirudiwe upya maana watu wwengi wanatamani kumuona.
Mchungaji huyo amesemakuwa wameamua kufanya tamasha hilo ndani ya ukumbi kwasababu ya kutii agizo la serikali na wao hawataki kupingana na serikali hivyo watajitahidi kulifanya tamasha hilo kwa mara ya pili ili watu wote waweze kufaidi .
Mchungaji huyo amesemakuwa wameamua kufanya tamasha hilo ndani ya ukumbi kwasababu ya kutii agizo la serikali na wao hawataki kupingana na serikali hivyo watajitahidi kulifanya tamasha hilo kwa mara ya pili ili watu wote waweze kufaidi .
Kwa upande wake Afisa Itifaki na uhusiano wa Aicc Rodney Thadeus amesema kuwa ukumbi huo unauwezo wa kuchukua watu 1350 hivyo usingeliweza kuhimili idadi kubwa ya watu ambao walitaka kuingia ukumbini hapo kwaajili ya tamasha hilo.
Martha Uhwelo Muimbaji wa nyimbo.za.injili ambaye hakufanikiwa kuingia ukumbini.
Kwa upande waimbaji ambao hawakufanikiwa kuingia ukumbini kwenye tamasha hilo wamesema kuwa waandaaji wa tamasha hilo hawajajipanga."Huwezi kumleta muimbaji mkubwa kutoka kundi.kubwa linalifahamika.duniani la Joyous Celebration kutoka Afrika ya Kusini ,kisha tamasha lifanyike ukumbini"
"Kila mtu amekuja hapa kwaajili ya kumunaona muimbaji Mkhululi Bhebhe,sasa ona tunaondoka hata ukumbini hatujaingia kwasababu ya ukumbi mdogo siku nyingine hawa waandaaji wakiandaa tamasha kama hili waliweke kwenye uwanja kila mtu afaidi alisisitiza mmoja wa aliyekuja kwaajili ya tamasha "
Muonekano wa ukumbi wa Simba ulivyofurika watu ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
Muimbaji Daniel Safari akiwa anaimba katika Tamasha hilo katika ukumbi wa Simba ndani ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)
Watu wakiwa nje ya Geti kuu AICC ambao wameshinndwa kuingia ndani ya ukumbi.
Sambamba na hayo kiongozi wa kundi la Worshipers Aberdnego Hango ambao ni wenyeji wa Muimbaji Mkhululi Bhebhe kutoka kundi la Joyous Celebration kutoka Afrika ya Kusini amesema kuwa tamasha hilo ni kubwa mno watu wamekuwa na muitikio mkubwa sana japo kuwa ukumbi umekuwa mdogo,amewataka wale ambao hawajafanikiwa kuingia ukumbini wasivunjike Moyo kwani season II inakuja hivi karibuni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni