.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 15 Agosti 2016

MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bw. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT. 

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa
wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko
Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti  2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland
ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa
kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia
uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya  Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha  miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini ya miradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa  masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa Halmashauri husika.
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bwa. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bwa. Peter Ireton
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar,Dkt Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni