Mwanamichezo wa China anayeshirikia
michuano ya Olimpiki amepata sapraizi ya maisha yake katika michuano
ya Rio 2016, baada ya mpenzi wake kumuomba kumvalisha pete ya uchumba
wakati wa hafla ya kupewa medali.
Mwanamichezo huyo wa kike He Zi, 25,
kutoka China alishinda medali ya fedha katika mchezo wa kuruka kwenye
maji huku ukipiga sakakasi katika umbali wa mita tatu jana, na
kujikuta akipewa zawadi kubwa ya pete ya uchumba.
Mpenzi wake Qin Kai, 30, alimpatia
sapraizi hiyo wakati akishuka kwenye jukwaa la kupokelea medalo,
ambapo alipiga magoti na kuongea nae kwa muda kabla ya kufungua
kisanduki kidogo kilichokuwa na pete, ambapo alikubaliwa.
He Zi akifunika uso kwa aibu baada ya kuambiwa "Utakubali kuolewa na mimi".
Qin Kai akifurahi baada ya He Zi kumkubalia kuolewa naye



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni