Wagonjwa na wauguzi wa hospitali ya
Mwingi nchini Kenya wameshtushwa baada ya mtu mwenye silaha kuingia
wodini na kumuua kwa kumpiga risasi mgonjwa aliyelazwa.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtu
huyo mwenye silaha alikimbia baada ya kumfyatulia risasi 17 mgonjwa
huyo huku wagonjwa wengine wakikimbia na kujificha chini ya vitanda
vyao.
Mgonjwa aliyeuwawa ametambulika kuwa
ni Ngandi Malia Musyemi, 27, aliyelazwa hospitali hiyo matibabu ya
majeraha ya risasi baada ya tukio la kutekwa gari.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni