.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 15 Agosti 2016

MWANAMKE AFUNGWA MIAKA KUMI KWA KUMUIBA MTOTO MIAKA 19 ILIYOPITA

Mahakama nchini Afrika Kusini imemuhukumu kifungo cha miaka 10 jela mwanamke mmoja aliyemuiba mtoto kutoka katika kitanda cha hospitali miaka 19 iliyopita na kumlea kama mtoto wake.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51 alikamatwa mwaka 2015 baada ya kubaini kufanana baina ya mtoto huyo wa kike Zephany Nurse na mtoto mwingine wa kike katika shule moja.

Vipimo vya DNA vilivyofanywa na polisi vilibaini kuwa watoto hao wa kike walikuwa ni ndugu.
          Zephany akiwa na mama yake mzazi hospitali kabla ya kuibiwa mwaka 1997
        Wazazi halisi wa Zephany wakikumbatiana baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni