Rais
wa Zambia Edger Lungu amechaguliwa tena kuwa rais, tume ya uchaguzi
ya nchi hiyo imetangaza matokeo hayo ambayo yamepingwa na wapinzani.
Tume
ya Uchaguzi Zambia imesema Lungu amepata kura asilimia 50.35, baada
ya uchaguzi huo uliofanyika Alhamisi, ikiwa ni zaidi ya asilimia 50
zilizohitajika kwa mujibu wa sheria.
Mpinzani
wake mkuu Hakainde Hichilema, ambaye alidai kufanyika kwa udanganyifu
katika upigaji kura amepata kura asilimia 47.67.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni