Baadhi ya vijana waliofika katika banda la wizara ya Kilimo na Mifugo wakipata maelezo juu ya ufagaji wa ng'ombe wa kisasa maalumu kwa ajili ya maziwa Dkt John Mpinga kutoka Luti Campus Tengeru
Na Dickson Mulashani. Vijana nchini wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo kilimo ikiwa ni sehemu ya kujikwamua na kuliletea Taifa maendeleo sambamba na kumuunga mkono Rais kwa kauli mbiu yake ya HAPA KAZI TU!. Hamasa hiyo inadhihirika wazi kupitia kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wakulima maarufu zaidi kama nanenane mwaka 2016 inayosema KILIMO MIFUGO NA UVUVI NI NGUZO YA MAENDELEO, VIJANA SHIRIKI KIKAMILIFU “HAPA KAZI TU” ambapo kitaifa yataadhimishwa mkoani Morogoro.
Mkulima wa zao la viazi vitamu akionesha namna viazi vinavyoweza kutengeneza bidhaa zaidi ya moja ikiwemo "tambi" na "crips"
Afisa wa kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa nishati kwa ajili ya matumizi ya nyumbani akielekeza namna mkaa unaotengenezwa kutumia pumba unavyofanya kazi
Mmoja wa waliotembelea banda la TAHA akiangalia kwa makini zao la Hoho iliyonona vyema ambayo ni sehemu ya mradi wa TAHA
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni