Zaidi ya abiria 282 na wafanyakazi 18 waliokuwa wakisafiri na shirika la ndege la Emirates wamenusurika kifo baada ya ndege hiyo kuanguka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai wakati ikitua.
Ndege hiyo Boeing 777 ilikuwa ikitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Trivandrum nchini India.
Taarifa za awali zinasema kuwa gia kwa ajili ya ndege kutua ilipata hitilafu. Wote walitoka salama baada ya ajali hiyo na hakuna taarifa zozote za majeruhi
Kufuatia ajali hiyo, uwanja huo kwasasa umefungwa hakuna ndege inayoruhusiwa kutua wala kupaa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni