Abiria wa ndege iliyokuwa ikielekea
Uingereza wameelezea namna walivyofikiria kuwa wanakufa, baada ya
ndege yao kuanza kupata mitikisiko ikiwa angani na kushuka chini hadi
futi 4,000.
Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la
Marekani aina ya Boeing 767-300 ikitokea Houston kwenda Haethrow
ililazimika kutua uwanja wa ndege wa Shannon nchini Ireland.
Ndege hiyo ilitua salama katika
uwanja huo, lakini watu 12 wakiwemo watoto watatu na wahudumu wawili
wa ndege walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Chuo Kikuu cha Limerick.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni