Mwanasoka shujaa wa Brazil katika
mchezo wa soka katika michuano ya Olimpiki, Neymar ameonekana
akishangilia timu ya mpira wa wavu ya wanaume ya Brazil katika mchezo
wa fainali ambao walishinda medali ya dhahabu.
Neymar, ambaye amejivua wadhifa wa
Kapteni wa Brazil, alifunga penati ya ushindi dhidi ya Ujerumani na
kusaidia Brazil kutwaa medali ya dhahabu pamoja na kulipa kisasi cha
kufungwa na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali za kombe la
dunia.
Timu ya mpira wa wavu ya Brazil
iliishinda Italia jana na kutwaa medali ya dhahabu na kuchangia
kuweka rekodi bora ya Brazil katika michuano hiyo kwa kutwaa medali
saba za dhahabu katika michuano hiyo ya Rio 2016.
Wachezaji wa mpira wa wavu wa Brazil wakishangilia ushindi


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni