Nyota wa filamu wa Bollywood, Shah
Ruh Khan, ametumia akaunti yake ya twitta kuonyesha kukerwa na
kitendo cha kushikiliwa kwa muda na mamlaka za Marekani katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Los Angeles.
Haikufahamika mara moja kwanini Khan
alishikiliwa katika uwanja huo wa ndege wa Marekani na ni kwa muda
gani.
Mwaka 2012, Wahindi walichukizwa
baada ya Khan kushikiliwa kwa dakika 90 katika uwanja wa White Plains
karibu na Jiji la New York.
Na mwaka 2009 Khan alishikiliwa kwa
muda wa saa mbili katika uwanja wa Newark na kuachiwa baada ya
Ubalozi wa India kuingilia kati.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni