Kocha ya wanamichezo wa riadha wa
Kenya waliopo Rio nchini Brazil amerudishwa nyumbani baada ya
kujifanya ni mwanariadha na kutoa sampuli ya haja ndogo kwa ajili ya
vipimo.
Kenya imesema kocha huyo John Anzrah
alijifanya ni mwanariadha wa mbio za mita 800 Ferguson Rotich na
kutia saini nyaraka za vipimo vya kubaini matumizi ya dawa
zilizopigwa marufuku.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya
Olimpiki Kip Keino amesema kuwa kamati yake haiwezi kuvumilia kitendo
hicho alichokifanya kocha huyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni