Oscar
ametikisa nyavu mara mbili, huku goli lake la kwanza likiwa la mkwaju
wa penati na la pili akimalizia vyema kwenye kona ya goli wakati
Chelsea ikishinda 3-1 dhidi ya AC Milan.
Katika
mchezo huo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi, Chelsea
ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Bertrand Traore kwa kichwa
baada shuti la Victor Moses kuokolewa.
AC
Milan ilisawazisha goli hilo kwa shuti la kuzungusha la mpira wa
adhabu lililopigwa kiufundi na Gianluigi Donnarumma na kufanya
matokeo katika kipindi cha kwaza kuwa 1-1.
Bertrand Traore akifurahi goli lake alilofunga
N’Golo
Kante aliingia dimbani na kuisaidia Chelsea kuwa imara kutokana na mchango wake mkubwa
Katika purukushani za soko dimbani Diego Costa alijikuta jezi yake ikichani mgongoni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni