Kiongozi
wa Kanisa Katoliki Papa Francis ameunda tume maalum kuangalia iwapo
kanisa hilo lianze kuruhusu kuwa na mashemasi wanawake.
Suala
hilo limekuwa lililisumbua kanisa kihistoria, huku wengi wakipinga
kuteuliwa mwanamke katika wadhifa huo.
Papa
Francis ameteuwa timu ya wanawake sita kutathimini suala hilo, na
kuangali jukumu la wanawake kihistoria katika miaka ya nyuma
kanisani.
Mashemashe
wanaruhusiwa kuhubiri, kufungisha ndoa na kuendesha ibada ya maziko
lakini hawaruhusiwi kuongoza ibada kanisani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni