JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
|
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia
salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa
Awamu ya Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na pia
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Aboud Jumbe
Mwinyi kilichotokea leo tarehe 14 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi na pia alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuanzia Mwaka 1972 hadi 1984.
Kufuatia
kifo hicho Rais Magufuli amesema Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye
alijitoa kupigania Uhuru, Umoja, Haki na Maendeleo ya Wananchi wa
Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika kipindi kigumu ambacho Taifa
lilikipitia.
"Nimeshitushwa
sana na kifo cha Mzee wetu Mhe. Aboud Jumbe, kwa hakika Tanzania
imepoteza mtu muhimu ambaye katika kipindi cha uongozi wake alitoa
mchango mkubwa wa kuipigania na kuijenga Tanzania tunayoiona leo"
Amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli ameendelea "Kupitia
kwako Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein napenda kuwapa pole familia ya Marehemu, Ndugu, Jamaa
na Marafiki wote, Wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote kwa ujumla
kwa kufikwa na msiba huu mkubwa".
Rais
Magufuli amemuombea marehemu Aboud Jumbe Mwinyi apumzike mahali pema
peponi.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es Salaam
14
Agosti, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni