Mjerumani
Toni Kroos ameifungia Real Madrid goli la ushindi dhidi ya Celta Vigo
katika mchezo uliomalizika kwa ushindi wa magoli 2-1.
Katika
mchezo huo, Alvaro Morata, aliipatia Real Madrid goli la kwanza mnamo
dakika ya 60, hata hivyo Fabian Orellana aliisawazishia Celta Vigo
kwa goli safi.
Toni
Kroos aliifanya Real Madrid iongoze kwa shuti la karibu katika dakika
ya 81 baada ya James Rodriguez aliyetokea benchi kutumia mwanya wa
makosa na kuchangia goli hilo.
Toni Kroos akiachia shuti lililoipa Real Madrid goli la ushindi
Mchezaji nyota wa Real Madrid Gareth Bale akiruka juu na kupiga mpira kwa kichwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni