.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 31 Agosti 2016

SAFARI YA TAIFA STARS KWENDA NIGERIA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anatarajiwa kuungana na timu hiyo nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).

Hadi mchana wa leo Agosti  29, 2016 ni Kelvin Yondan pekee kutoka Young Africans ambaye hakuripoti kwenye kikosi hicho kilichopiga kambi yake kwenye Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kipa mpya wa timu hiyo, Said Kipao alijiunga na timu hiyo mara moja baada ya kuteuliwa na Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.

Taifa Stars inatarajiwa kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super Eagles utakaofanyika Septemba 3, 2016. 

Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon, lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa katikati ya mashindano.
Wachezaji wanaotarajiwa kuondoka ni:

Makipa-
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC

Mabeki
Kelvin Yondani - Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
Shomari Kapombe - Azam FC
David Mwantika - Azam FC

Viungo
Himid Mao - Azam FC
Shiza Kichuya – Simba SC
Ibrahim Jeba – Mtibwa Sugar
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Juma Mahadhi - Young Africans
Farid Mussa Tenerif ya Hispania

Washambuliaji
Simon Msuva - Young Africans
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC

Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni