Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji Jumapili ya Septemba 4, 2016
inatarajiwa kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Hassan Ramadhan Kessy
anayedaiwa na Klabu ya Simba kuvunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi
na klabu ya Young Africans sambamba na kusajili katika timu hiyo ya Mtaa
wa Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mkataba wake kufika mwisho Juni 15,
2016.
http://tff.or.tz/news/563-kama ti-ya-katiba-sheria-na-hadhi- za-wachezaji
Kwa
mujibu wa CECAFA, michuano hiyo itafanyika jijini Jinja na Tanzania
ambayo inaongoza kwa ubora wa viwango vya Mpira wa Miguu kwa nchi za
Afrika Mashariki imepangwa kundi B ikiwa pamoja na timu za Rwanda na
Ethiopia wakati kundi A litakuwa na timu za Kenya, Burundi, Zanzibar
pamoja na mwenyeji Uganda.
TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TANZANIA BARA
Shirikisho
la Mpira Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kwa Shirikisho la Vyama
vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), kuwa timu ya taifa
ya wanawake ya Tanzania itashiriki michuano ya kwanza ya Kombe la
Chalenji kwa wanawake itakayofanyika kuanzia Septemba 11, 2016 hadi
Septemba 20, 2016 kwa kushirikisha nchi saba wanachama wa shirikisho
hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni