Mshambuliaji
wa Manchester City Sergio Aguero ameachwa katika kikosi cha Argentina
cha kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 kutokana na kuwa
majeruhi.
Chama
cha Soka cha Argentina kimethibitisha kuwa Aguero alipata jeraha
katika mchezo wa ligi ambao City ilishinda magoli 3-1 dhidi ya West
Ham jumapili.
Haijaelezwa
ni lini Aguero ataitwa tena kikosini, pia kwa upande mwingine huenda
akakabiliwa na adhabu ya FA kwa kumpiga kiwiko beki wa West Ham,
Winston Reid.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni