Serikali ya Bolovia imesema naibu
waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ametekwa na kuuwawa na wachimba
madini waliokuwa kwenye mgomo.
Waziri huyo Rodolfo Illanes na
mlinzi wake walitekwa siku ya Alhamisi kwenye kizuizi cha barabarani
eneo la Panduro, kusini mwa La Paz.
Waziri wa Mambo ya Ndani Carlos
Romero amesema kuna kila dalili kuwa Bw. Illanes ameuwawa kwa
kushambuliwa kikatili.
Wachimbaji madini wawili nao
wamekufa kwa majeraha ya risasi baada ya kupambana na polisi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni