Kocha mgumu wa kutoa fedha za
kununua wachezaji Arsene Wenger ametumbukiza mkono mfukoni na kutoa
kitita cha paundi milioni 50 kuwanasa wachezaji beki Shkodran Mustafi
na mshambuliaji Lucas Perez, kabla ya muda wa usajili haujaisha.
Ombi la Arsenal ambayo imeanza kwa
kusuasua katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Uingereza limekubaliwa na
wachezaji hao wawili, na sasa inaamini kuwa itafanikisha kukamilisha
mpango huo kabla ya kufungwa kwa usajili jumatano.
Iwapo mpango huo utakamilika
unatarajiwa kupunguza shinikizo kwa Wenger ambaye mashabiki wa
Arsenal wamekuwa wakishikiza kuboreshwa kwa kikosi baada ya kuambulia
pointi moja tu katika michezo yao miwili ya Ligi Kuu.
Beki wa kati wa Valencia Shkodran Mustafi ambaye Arsenal wanamuwania
Mshambuliaji wa Deportivo La Coruna Lucas Perez kulia anawaniwa na Arsenal
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni