.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Agosti 2016

WANANCHI WASIRUBUNIKE NA TAASISI FEKI ZA MRADI WA MILIONI 50

NEEC1
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Bi. Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafanyakaz wa baraza hilo hawapo pichani alipozungumzia kuhusu mkakati wa mradi wa Milioni 50 zitolewazo na Serikali kwa kila kijiji leo jijini Dar es salaam.
NEEC2
Baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) wakifatilia kwa kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa (NEEC) Bi. Beng’i Issa hayupo pichani alipozungumzia kuhusu mkakati wa mradi wa Milioni 50 zitolewazo na Serikali kwa kila kijiji leo jijini Dar es salaam.
 

                                                                                              Abushehe Nondo-Maelezo

Wananchi wametakiwa kuwa makini na mtu au taasisi binafsi zinazopita na kuwadanganya kwa kuwatoza fedha za usajili wa kikundi kwa ajili ya kufaidika na mpango wa Millioni 50 kwa kila kijiji kama zilivyoahidiwa na Serikali ya awamu ya tano.

Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa amesema kuwa kuna taasisi binafsi zimejitokeza na kuwatoza fedha za usajili wa kikundi ili kuweza kufaidika na mradi huo kinyume na taratibu za Serikali.

Bi. Issa amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na taarifa kutoka sehemu mbalimbali nchini kuwa baadhi ya taasisi na watu binafsi wanawadanganya wananchi kuwa mpango wa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji zitapitia kwenye taasisi zao na kuwatoza wananchi fedha za usajili.

“Wananchi wasirubuniwe na kutoa fedha za usajili kwa ajili ya kupata fedha za mradi huo kwani hakuna malipo yoyote na bado ugawaji huo haujaanza” alisema Bi. Issa.

Aidha Bi. Issa amesema kuwa mradi huo bado haujaanza kutolewa kwa kuwa Serikali bado inapanga utaratibu wa kuwafikia wananchi wa vijiji vyote nchini ili kunufaika na mradi huo.

Mbali na hayo Bi. Issa ametoa rai kwa watanzania wasihadaike na taasisi hizo na kutoa onyo kali kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na zoezi hilo hatua kali zitachukuliwa zidi yake.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni