.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Agosti 2016

ZIARA YA MAJALIWA INYONGA WILAYANI MLELE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa wodi katika zahanati ya Inyonga wilayani Mlele amabayo inatarajiwa kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya . Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kisalimiana na viongozi wa wilaya ya Mlele wakati alpowasili kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 22,2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakimsikiliza Chifu Kayamba wa Pili (kulia) wakati Waziri Mkuu alipotwazwa kuwa Chief wa Wakonongo na kupewa jina la Kayamba wa Kwanza katika mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga wialyani Mlele Agosti 22, 2016.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa Inyonga baada ya waziri Mkuu kutawazwa kuwa Chief wa Wakonongo na kupewa jina la Chief Kayamba wa Kwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Inyonga Agosti 22, 2016. Kulia ni Cheif wa Wakonongo, Kayamba wa Pili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Katavi, Mhandisi Isaack Kamwelwe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Inyonga wilayani Mlelele Agosti 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Inyonga wilayani Mlele Agosti 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni