Wanawake
ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondolewa kidole tumbo ama
mafindofindo wamebainika kuwa na uwezo mkubwa wa kutunga ujauzito,
utafiti wa miaka 15 umebani hilo.
Watafiti
wa Chuo Kikuu cha Dundee, walifanyia tathimini za kumbukumbu za
utabibu kwa zaidi ya nusu ya wanawake nusu milioni.
Watafiti
hao wa tiba wamesema ufanyaji upasuaji wa kuondolewa viungo hivyo
mwilini unaweza kusababisha moja kwa moja hali hiyo ama huenda
ni kutokana na mabadiliko ya tabia.
Wataalam
hao wamesema matokeo hayo yanaweza kusaidia kuibua tiba mpya ya
ugumba, lakini wamewashauri wanawake wasifanye upasuaji wa kidole
tumbo ama mafindofindo bila sababu za msingi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni