.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 9 Agosti 2016

WAZIRI NAPE AWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUANDIKA HABARI ZA MAENDELEO YA BARA LA AFRIKA

bal3
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la Afrika na China.
bal4
Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing akiwasilisha hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam ulikuwa ukijadali masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bara la Afrika na China.
bal5
Mshauri wa mambo ya Mawasiliano kutoka Tume ya Umoja wa Afrika Bibi. Doreen Apollos akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.

bal1
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (Kushoto) akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
bal2
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katika) akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Bw.Lv Youqing.

bal6
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing(kulia) wakati wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejikita katika kujadili uhusiano wa Afrika na China kupitia Nyanja mbamilmbali ikiwemo mawasiliano na afya.
bal7
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (wa kwanza kulia) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing(wa pili kulia) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye(hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
bal8
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) na Balozi wa China nchini Bw. Lv Youqing (kulia) wakionyesha hundi ya shilingi milioni arobaini na tano zilizotolewa na watu wa China kwa ajili ya kuchangia madawati katika shule za msingi za Dar es Salaam.
bal9
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye (katikati waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam.
bal10
Wajumbe wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum leo jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.

                                                                                      Na Lorietha Laurence-WHUSM

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Mosses Nnauye amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa kuandika habari za maendeleo ya bara la Afrika.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum na kueleza kuwa uhusiano baina ya Afrika na China ni wa muda mrefu na umejikita katika kuboresha teknolojia ya mawasiliano na hivyo kukuza uchumi wake.

Aidha aliongeza kuwa ili bara la Afrika liweze kuelezea historia yake kwa mataifa mingine katika kujiletea maendeleo kuna haja ya kuvijengea uwezo vyombo vya habari katika kutoa habari nzuri zenye manufaa kwa jamii husika.

“Katika karne hii tuliyopo sasa kuna mabadiliko mengi ya teknolojia hivyo ni budi kuendelea kuimarisha ushirikiano ulipo baina ya China na Afrika ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii zetu kupitia vyombo vya habari huku tukitunza na kueneza tamaduni zetu” alisema Mhe.Nape.

Waziri Nape alizidi kufafanua kuwa vyombo vya habari katika nchi za bara la Afrika vina uwezo mkubwa wa kukuza na kueneza utamaduni, kuhudumia jamii,kujenga umoja wa kitaifa na kulinda maslahi ya jamii duniani.

Naye Rais wa China Public Diplomacy Association Bw. Li Zhaoxing amesema kuwa anafurahishwa na uhusiano uonaozidi kuimarika baina ya nchi za Afrika na China na kuahidi kuboresha mawasiliano na mahusiano ili kufikia mafanikio makubwa yaliyokusudiwa.

Mkutano wa China-Afrika Public Diplomacy Forum umejikita katika kujadili mambo mbalimbali ikiwemo mahusiano baina ya mtu na mtu na Vyombo vya habari,afya,na tiba asilia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni