Utafiti mpya umelaumu ongezeko la
joto kwa karne moja iliyopita kuwa ni chanzo cha kushuka kwa mavuno
ya uvuvi katika moja ya ziwa muhimu kwa uvuvi duniani.
Ziwa hilo ambalo ni Ziwa Tanganyika
ni miongoni mwa maziwa ya muda mrefu Afrika ambalo samaki ni mlo
muhimu kwa mataifa ya jirani na ziwa hilo.
Hata hivyo mavuno ya samaki
yamepungua katika miongo ya hivi karibuni wakati uvuvi wa kibiashara
ukiongezeka.
Hata hivyo utafiti huo mpya umesema
ongezeko la joto ndio chanzo kikuu cha tatizo la kupungua samaki Ziwa
Tanganyika na wala si ongezeko la uvuvi wa samaki.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni