Mpira
wa adhabu uliopigwa na Xherdan Shaqiri umeipatia Stoke City pointi
moja na kuinyima ushindi waliostahili timu ya Middlesbrough katika wa
Ligi Kuu ya Uingereza.
Boro
walikuwa wanaongoza baada ya kuwashusha dimbani wachezaji wake wawili
kati ya 10 waliowasajili baada ya kupanda daraja, na alikuwa Alvaro
Negredo aliyeandika goli la kwanza.
Xherdan Shaqiri akishangilia kwa aina yake goli la alilofungwa kwa mpira wa adhabu na kuisawazishia Stoke City
Katika
mchezo mwingine mpira wa kichwa uliopigwa na Erik Lamela katika
kipindi cha pili uliipatia pointi moja Tottenham dhidi ya Everton
ambao wameonyesha kuvutia wakiwa chini ya kocha Ronald Koeman.
Everton
walianza kwa kuishambulia sana Spurs ambayo ilionekana kupwaya katika
kipindi cha kwanza na kupata goli la kuongoza kupitia mpira wa adhabu
uliopigwa na Ross
Barkley.
Mpira wa adhabu uliopigwa na Ross
Barkley ukimshinda kipa Hugo Lloris




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni